Breaking News

Breaking News: Ndege yatoweka angani ikiwa na abiria 100



Ndege moja ya jeshi la Burma, iliyokuwa imewabeba zaidi ya watu 100, imetoweka angani.
Hayo ni kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa wakuu wa nchi hiyo.

Ndege hiyo ya kijeshi, ilikuwa ikipaa kati ya Yangon (Rangoon) na mji ulioko kusini mwa nchi hiyo wa Myeik. Shughuli za kutafuta na kuokoa manusura zinaendelea.

"Tulipoteza mawasiliano na ndege hiyo mwendo wa saa nne na dakika 35 leo asubuhi saa za Afrika Mashariki [07:05 GMT], pale ndege hiyo ilipofika maili 20 magharibi mwa mji wa Dawei," jeshi la Burma limesema kwa njia ya taarifa.

Kulikuwa wana abiria 105 na wafanyikazi 11 kwenye ndege hiyo, duru kutoka uwanja wa ndege zimeiambia shirika la habari la AFP.

Aidha, jeshi la nchi hiyo halijasema ni watu wangapi walikuwa ndani ya ndege hiyo ya mizigo iliyoundiwa China.

Ndege za wanajeshi pamoja na helikopta zimetumwa katika eneo hilo katika shughuli za kuwatafuta manusura au mabaki ya ndege hiyo ambayo kufikia sasa inaaminika kuwa imeanguka.

Taarifa inaongeza kuwa, ndege hiyo ilikuwa angani ikivuka bahari ya Andaman, pale ilipotoweka.

No comments