Breaking News

BREAKING NEWS; POLISI WAPIGA MABOMU YA MACHOZI,MAJI YA KUWASHA KUTAWANYA WAENDESHA BODABODA SAKATA LA KIFO CHA MWENZAO SHINYANGA


Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limetumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwasambaratisha waendesha bodaboda mjini Shinyanga waliokuwa wamefunga barabara kuu ya Shinyanga – Tabora wakidai askari wa jeshi hilo amesababisha kifo cha mwendesha bodaboda mwenzao- SOMA <<HAPA>>


Mabomu ya machozi yameanza kupigwa leo Jumatano June 7,2017 tangu asubuhi mpaka majira ya saa sita mchana  katika mitaa mbalimbali mjini Shinyanga.

Wakati polisi wakipiga mabomu,wananchi,waendesha bodaboda nao walikuwa wanajibu mashambulizi kwa kuwarushia mawe askari polisi.


Pamoja na jeshi hilo kupiga mabomu, limekwenda hadi nyumbani kwenye msiba alipokuwa akiishi marehemu na kuwatawanya kwa kuwakamata bodaboda na pikipiki zao hali iliyozua taharuki zaidi.

Inaelezwa kuwa waendesha bodaboda hao wamegoma kumzika mwenzao wakishinikiza mpaka mkuu wa mkoa afike nyumbani kwa marehemu.
           TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUWALETEA HAPA HAPA MASANGULATZ BLOG 0742532203

malunde1 blog, vurugu shinyanga

No comments