Jeshi siyo chombo kinachoweza kuajiri vijana uchochoroni” – JWTZ
“
Siku za hivi karibuni kuweibuka watu wanaodai kuwa ni Maofisa wa JWTZambao wamekuwa wakiwatapeli watu kwa kudai kuwa na uwezo wa kuwaingiza kwenye Jeshi la Kujenga Taifa JKT na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZmoja kwa moja bila mchakato wowote.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Utumishi wa JWTZ Major Jenerali Harrison Masebo amesemaJWTZ lina mchakato wa kuwapata Askari wanaotambulika kutoka JKT na sio mtaani hivyo amewataka wananchi kujiepusha na matapeli hao.
“Kuna vikundi ama watu ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakijitangaza kwamba wao wana uwezo wa kutoa nafasi za kujiunga kwenye mafunzo ya JKT…wamekuwa wakijitangaza kwamba wao wana uwezo wa kuwaajiri vijana moja kwa moja kujiunga na Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania. Vikundi hivyo msivisikilize sio vikundi rasmi ama watu hao si watu rasmi.”
Kwa upande mwingine JWTZ limesisitiza kuwa limekuwa mara kwa mara likitoa ufafanuzi juu ya namna ya kujiunga na mafunzo ya Jeshi hilo likisema kuwa zipo taratibu maalum zilizowekwa kujiunga kwa ajili mafunzo: “Jeshi limekuwa likifafanua mara kwa mara. Jeshi la Ulinzi wa Wananchi na JKT mara kwa mara limekuwa likifafanua kuhusu taratibu za kujiunga nafasi za mafunzo ya JKT na taratibu za kujiunga na Jeshi la Ulinzi wa Wananchi.” – Major Jenerali Harrison Masebo.
No comments