Bandari bubu zaendelea kuitesa Serikali
Kauli hiyo imetolewa leo (Ijumaa) na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani ambaye amesema Serikali pekee haitaweza kukomesha suala hilo kama hakutakuwa na ushirikiano kutoka kwa wananchi
Serikali imekiri kuwepo kwa bandari bubu nyingi na kueleza kuwa ndizo zinazosababisha uwepo wa uhalifu na usafirishshwaji wa mizigo kinyume cha sheria.
Kauli hiyo imetolewa leo (Ijumaa) na Naibu Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani ambaye amesema Serikali pekee haitaweza kukomesha suala hilo kama hakutakuwa na ushirikiano kutoka kwa wananchi.
Ngonyani ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Temeke(CUF), Abdalah Mtolea.
Ngonyani amekiri Serikali haina idadi kamili ya bandari bubu lakini imekuwa ikishughulika na wahalifu kwa kuwasaka na kuyatambua maeneo hayo ambayo pia yanatumika kukwepa kodi.
No comments