Breaking News

MBUNGE ELIBARIKI KINGU AFAFANUA KAULI YAKE ILIYOIBUA UTATA KUHUSU WATU KUTEKWA


Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu amefafanua kuhusu kauli iliyosambaa mtandaoni ikidai kuwa amesema watu kutekwa na kuuawa ni jambo la kawaida na kushauri bunge kutounda tume kuchunguza kwani itazua taharuki na Serikali haijashindwa kusimamia usalama wa nchi.

“Sijasema kutekwa kwa watu ni matukio ya kawaida, mimi nimesema matukio ya kihalifu yapo Duniani kote, tusilipake taifa matope ili lionekane limekuwa katika hali tete, hatuwezi kuanza kwenda kujadili hali ya usalama kwa matukio haya,” -Kingu

No comments