MEYA WA KINONDONI ANAKUPATAARIFA HII MUHIMU
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Slaam, imeanza utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa kiwanda cha mbolea chenye kutumia malighafi ya taka za kwenye masoko.
Zaidi ya sh.bilioni 4.1 zinatarajiwa kutumika katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda hicho kitakachojengwa katika eneo la Mabwepande.
Mradi huo unajengwa kwa ushirikiano wa wa Serikli ya Ujerumani kupitia jiji la Humburg na serikali ya Tanzania kupitia jiji la Dar es Saaam.
Kata makubaliano kati ya majiji la haya mawili Jiji la Humburg litaghramia ujenzi wa mradi huo na kuuendesha kwa muda wa mwaka mmoja ambapo itahusika pia katika kujenga uwezo wa wataalamu wa manispaa katika uendeshaji wa kiwanda.
Akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa mradi huo, Dar es Salaam, jana, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta, alisema jiji la Humburug litatoa sh.bilioni 2.78 na sh.bilioni 1.32 zitatolewa na serikali kuu ya Ujerumani.
‘’ Chini ya makubaliano hayo Msanispaa ya Kinononi itagharamia upatikanaji wa kiwanda na tayari ekari 14 zimepatikana.Pia Manispaa itagharamia miundombinu ya barabara, maji na umeme kiwandani,’’alisema Meya Sitta.
Aliongeza: ‘’Ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kuanza mapema mwezi huu na taratibu za ununuzi na kumpat mkandarasi wa ujenzi zipo katika hatua za mwisho.Ujenzi utachukua miezi 12,’’
Alisema radi huo utakapokamilika utakuwa na faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupunguza taka za kwwenye masoko .
‘’Wastani wa tani 180 za taka huzalishwa kila siku katika masoko yaliypo ndani ya Manispaa ya Kinondoni na uwezo wa wa kiwanda ni kuchakta taka tani 50 kwa siku .Kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 25 za mbolea kwa siku,’’alieleza Meya huyo.
Alitaja faida zingine kuwa ni kuongeza mapato ya Manispaa kutokana na mauzo ya mbolea, kupunguza matumizi ya mbolea zenye kuleta athari kwenye ardhi na afya za binadamu pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa watanzania.
Alisema utekelezaji wa mradi huo awali ulisimama kutokana na Manispaa hiyo kusaini mkataba wa utekelezaji moja kwa moja na jiji la Humburug, hali ambayo kiutaratibu ilifanya serikali kushindwa kuondoa kodi.
Kwa upande wa Mwakilishi wa Jiji la Humburg Dk. Florian Koelch alisema, kiwanda hicho kitajengwa katika eneo la heka mbili litakalosakafiwa na litahifadi taka kwaajili ya kuozeshwa ambalo litakuwa salama kwa unyevu
‘’Hatua hii ya mwanzo huchukua wiki mbili na baada ya hapo taka zisizooza huhamishiwa sehemu maalumu. Mchakato wa uozeshaji taka huchkuaa wiki nane hadi 10. Mradi huu utasajiliwa kama mradi wa kulinda mazingira chini ya ya tasisi ya The gold standard –GS’’ alisema Koelch.
Mradi huo utasimamiwa na kampuni ya Atmosfair ya nchini Ujerumani.
No comments