TEMEKE YAELEMEWA NA IDADI KUBWA YA WANAFUNZI
UONGOZI wa Manispaa ya Temeke jijiniDar es Salaam, umetangaza kuelemewana idadi kubwa ya wanafunzi zaidi ya 27,000 walioandikishwa darasa lakwanza mwaka huu.
Imeelezwa kuwa kutokana na hali hiyo,madarasa yanatumika kwa zamu.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, NaseebMmbaga, alibainisha hayo jana wakatiakipokea msaada wa saruji mifuko 100kutoka Chama cha Madereva wa mabasiyaendayo Kusini (Umakuta).
Alisema makadirio yalikuwakuandikisha watoto 22,000, lakinikumekuwapo na ongezeko la wanafunzizaidi ya 5,000.
Alisema yanahitajika madarasa mapya90, ili wanafunzi wote wakae darasanikwa wakati mmoja na kuondokana nautaratibu wa kusoma kwa zamu.
Kwa upande wa sekondari, Mmbagaalisema kuna ongezeko la mahitaji yamadarasa mapya 130, kati ya hayo 90yapo katika hatua ya mwisho ujenziwake kukamilika.
“Halmashauri imeelemewa na idadikubwa ya wanafunzi waliondikishwadarasa la kwanza, tumeamua kuwekautaratibu wa kusoma kwa zamu katika shule zote, ili kukabiliana na wingi wa wanafunzi wakati tunaendelea kutafuta mbinu ya kutatua ikiwamo kujenga madarasa na shule mpya,” alisema Mmbaga.
Alipongeza hatua ya madereva hao kutoa msaada wa saruji kwa ajili ya kuongeza kasi ya ujenzi wa madarasa ili kukabiliana na ongezeko hilo.
Mbaga, alisema kama wadau wataendelea kujitolea pamoja na Manispaa kuweka nguvu zake, ana matumaini itakapofika Machi madarasa yote yatakamilika na kurejea katika hali ya kawaida.
Katibu wa Umakuta, Yusuph Malabe, alisema wao kama madereva ambao pia wazazi wameguswa na tatizo hilo na kwa umoja wao wameamua kutoa msaada huo wa saruji.
“Tumeguswa na tatizo hili, baada ya kujadiliana na Mkurugenzi tunaweza kusaidiaje, tumeona tutoe mifuko ya saruji katika kusukuma ujenzi wa madarasa mapya,” alisema Malabe.
No comments