Breaking News

NDALICHAKO AFANYA ZIARA CHUO CHA KAMPALA ABAINI KUWEPO KWA WALIMU WANAOISHI BILA VIBALI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amefanya ziara Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), kubaini baadhi ya walimu kuishi nchini bila vibali.

Katika ziara hiyo iliyofanyika leo Februari 20, 2018 Profesa Ndalichako ameambatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Anna Makakala, mkuu wa Ithibati na Udhibiti Ubora wa Vyuo, Dk Valerian Damian na maofisa mbalimbali kutoka idara ya uhamiaji na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Profesa Ndalichako amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwamo walimu wa chuo hicho kuajiriwa sehemu zaidi ya moja na kuishi nchini bila vibali.

"Wapo walioingia nchini kama wanafunzi lakini baada ya muda wakaajiriwa kama wafanyakazi, hii kwa sheria za nchi haikubaliki,” amesema Profesa Ndalichako.

No comments