Breaking News

SPORTPESA YAFUTA UDHAMINI KWA TIMU ZA KENYA

Kampuni ya michezo ya ubashiri ya SportPesaleo Jumanne ya January 2 2018 kupitia kwa mtendaji Mkuu wake nchini Kenya Ronaldo Karauri wametangaza kufuta udhamini katika michezo mbalimbalu nchini Kenya kwa kigezo cha kuongezewa tozo la kodi kwa asilimia 35.

SportPesa wamefuta udhamini katika michezo yote iliyokuwa imedhamini nchini Kenya kwa madai ya kuzidishiwa tozo la kodi lakini piaSportPesa kupitia kwa CEO Ronaldo Karauri amethibitisha kuwa  watapunguza matangazo ili kuipunguzia kampuni gharama za uendeshaji.

Maamuzi hayo ya SportPesa yataviathiri vilabu vya Gor Mahia, AFC Leopards na Nakuru All Stars ambavyo vilikuwa vimedhaminiwa na kampuni hiyo lakini pia itaathiri Ligi Kuu Kenyaambapo SportPesa alikuwa mdhamini Mkuu katika Ligi hiyo inayoshirikisha timu 18, Kenya Boxing League na rugby.

No comments