Breaking News

ZITTO KABWE AVUTIWA NA NIKI WA PILI

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameonyesha kutamani kufanya siasa na msanii wa bongo fleva, Niki wa Pili ambaye amekuwa na msimamo wake juu ya mambo mbalimbali ambayo yanaendelea nhini kwa sasa. 

Zitto Kabwe amesema hayo kupitia mtandao wake wa Twitter wakati akijibu moja ya jumbe ya msanii huyo ambapo alikuwa akielezea juu ya ushindani wa uchaguzi uliopita ambao ulikuwa na mvuto wa aina yake kuanzia kwenye mikutano ya kampeni, ambapo mamia ya wananchi walikuwa wakifurika kwenye mikutano hiyo na kusema kero za wananchi ndizo zilipelekea watu wengi kujitokeza katika kampeni hata kupiga kura. 

"Ushindani wa uchaguzi ulio pita na tsunami na mafuriko ulikuwa ni wingi wa wananchi na kero zao, tusiutafsiri kwa maana ya wanasiasa na kuwapa uhodhi wao, kama ulikuwa ni ushindani wao" aliandika Niki wa Pili 

Kufuatia hoja hiyo ya Niki wa Pili ndipo hapo aliibuka Zitto Kabwe na kusema kuwa siasa za Tanzania zinahitaji watu wenye misimamo ya kiitikadi na bahati mbaya zaidi watu wenye misimamo hiyo wamekuwa hawataki kuingia kwenye siasa. 

"Kaka siasa zetu zinakosa wanasiasa wenye 'convictions' ( sijui Kiswahili chake) kwa sababu watu kama wewe mwenye misimamo ya kiitikadi hamtaki kujiunga na vyama. Njoo tufanye kazi ngumu lakini muhimu ya kujenga siasa zinazoondoa uhodhi kwa wanasiasa" aliomba Zitto Kabwe

No comments