Breaking News

ZANZIBAR HEROES KUMKOSA HAJI MWINYI KWENYE MCHEZO WA LEO



Zanzibar inashuka dimbani leo kuivaa mabingwa watetezi Uganda katika mechi ya nusu fainali ya Chalenji ikiwa inamkosa beki wake wa kushoto, Haji Mwinyi.

Zanzibar Heroes itamkosa Haji kutokana na kuwa kadi za njano zinazomlazimisha kukaa jukwani na Kocha Mohammed Morocco amethibitisha.

Hata hivyo, Morocco amesema wamejipanga kufanya vema kwa kuwa wana kikosi kipana.

“Tuna kikosi kipana, kuna watu watakaomuwakilisha Haji pamoja na wengine walio majeruhi,” alisema.

 

Zanzibar Heroes ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano hiyo baada ya Tanzania Bara kuonekana “mdebwedo” kwa kung’olewa mapema kabisa.

No comments