Takwimu: Watu Bilioni 1.7 Huugua Magojwa ya Kuhara
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu amesema kuwa Takwimu za shirika la Afya duniani linaonyesha kuwa kila watu wapatao Bilioni 1.7 huugua magonjwa ya kuhara ambapo watu bilioni 1.8 hupoteza maisha ikiwa ni sawa na kupoteza watu wanne kila dakika duniani kote.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo, mjini Dodoma katika uzinduzi wa Kampeni Taifa ya Usafi wa Mazingira awamu ya pili inayobeba jina la ‘Usichukulie poa – nyumba ni choo’
“Takwimu za shirika la Afya duniani linaonyesha kuwa kila watu wapatao Bilioni 1.7 huugua magonjwa ya kuhara, ambapo watu bilioni 1.8 hupoteza maisha, ikiwa ni sawa na kupoteza watu wanne kila dakika duniani kote takiwimu za hapa nchini zinaonyesha watu wapatao 30,000 na baadhi yao hupoteza maisha,” amesema Makamu wa Rais.
“Hali ya usalama wa haki za binadamu haiko vizuri, na tutarekebisha endapo tutazingatia usafi wa mazingira na nimefurahi sana kuwa idai kubwa ya watoto wa shule wapo hapa hawa ndio wanaopaswa kuyasikiliza haya kwasababu wanasema samaki mkunje angali mbichi.”
No comments