ASKARI POLISI AMTWANGA RISASI MPENZI WAKE AMBAE NI MWANAJESHI HUKO MAKAMBAKO
Katika mji Mdogo wa kibiashara uitwao Makambako ulio mkoani Njombe asubuhi ya leo Askari polisi ajulikanae kwa majina ya Zakayo Dotto Kileka amemtwanga risasi na kumsababishia umauti mpenzi wake ambae ni mwanajeshi ajulikanae kwa jina la Neema.
Neema alikua akifanya kazi JWTZ Camp ya Makambako na Zakayo ni askari Polisi Makambako.
Inasemekana Zakayo alichukua silaha kituoni asubuhi ya leo tayari kwa kwenda lindo katika benk ya NBC Makambako na ndipo aliponyoosha hadi nyumbani kwa neema na kumsababishia umauti huo.
Zakayo ametoroka na juhudi za kumsaka zinaendelea. Chanzo cha ugomvi hakijajulikana bado zaidi ya kuhisiwa kua ugomvi wa mapenzi.
No comments