TETESI ZOTE ZA USAJILI ULAYA NIMEKUWEKEA HAPA
habari kuu za uhamisho kutoka Ligi ya Uingereza, La Liga, Serie A na ligi nyingine dirisha lausajili linapoelekea kufungwa Uingereza
SHAW MBIONI KUONDOKA UNITED
Manchester United wapo mbioni kumtoa Luke Shaw kwa mkopo dirisha la uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa The Sun .
CITY WAANDAA DAU LA BERTRAND
BARCELONA KUANZA UPYA KUMFUKUZIA COUTINHO JANUARIPAUL POGBA APATA MAJERAHA MAN UNITED IKISHINDA DHIDI YA BASELNEYMAR AMEONYESHA NI KWA NINI PSG WALIMSAJILI - ALVESDIEGO COSTA: "ANTONIO CONTE HANA HAIBA"
Manchester City wapo tayari kutoa dau la puandi milioni 30 kwa ajili ya nyota wa Southampton Ryan Bertrand, kwa mujibu wa The Sun .
CAN KUONDOKA BURE LIVERPOOL?
Emre Can anaelekea kuwa mchezaji huru baada ya mazungumzo yake na Liverpool kuhusu mkataba mpya kuenda mrama, limedai Daily Mail .
KANE ASUKUMIWA REAL MADRID
Real Madrid wanashinikizwa kumsajili nyota wa Tottenham Harry Kane na wasambazaji wa fulana Adidas, kwa mujibu wa Don Balon.
TORRES KUONDOKA ATLETICO JANUARI
Mshambuliaji wa Atletico Madrid Fernando Torres yupo mbioni kuihama klabu hiyo uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa Cadena SER .
CONTE & ABRAMOVICH HAWAONGEI
Mahusiano baina ya meneja wa Chelsea Antonio Conte na mmiliki Roman Abramovich yamevurugika kiasi ambacho hawaongei tena, limeripoti Marca.
CITY IPO TAYARI KUTOA €400M KUMSAJILI MESSI
Manchester City wapo tayari kutoa dau la euro milioni 400 kwa ajili ya Lionel Messi Januari ikiwa ataamua kutosaini mkataba Barcelona, kwa mujibu wa AS .
PSG YAMTENGEA DAU LA €150M COUTINHO
Paris Saint-Germain wapo tayari kuipiga vita Barcelona kumsajili kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho kwa mujibu wa Sport .
JAMES RODRIGUEZ ANATAKA KURUDI MADRID
James Rodriguez anataka kurudi Real Madrid kufuatia kutupiwa virago kwa Carlo Ancelotti na Bayern Munich, kwa mujibu wa Diario Gol .
LIVERPOOL YADAI £1BILIONI KUANZA MAZUNGUMZO KUUZA KLABU
Wamiliki wa Liverpool wameingia kwenye mazungumzo ya kuuza klabu hiyo, lakini klabu inataka inataka kulipwa paundi bilioni moja kuanza kuachilia klabu hiyo, kwa mujibu wa The Sunday Mirror .
ARSENAL & BARCA KUCHUANA KUMSAJILI MARTIAL
Anthony Martial ni mchezaji ambaye Arsenal na Barcelona zinataka kupigana vikumbo kumsajili kutoka Manchester United kwa mujibu wa habari.
Mirror limeripoti kuwa Arsenal wanahisi Mfaransa huyo anaweza kuwa mrithi sahihi wa Alexis Sanchez, wakati Mundo Deportivo limedai kuwa Barca wameonyesha kuvutiwa na uwezo wa mchezaji huyo.
AC MILAN YAMTAKA AGUERO AGUERO
Manchester City wakiwa wanaandaa dau la paundi milioni 20 kwa ajili ya Alexis Sanchez Januari. AC Milan wanajipanga kumsajili Sergio Aguero, kwa mujibu wa Daily Mail .
Ripoti zinadai kuwa Pep Guardiola yupo tayari kumruhusu Sergio Aguero kuondoka ikiwa atampata Alexis Sanchez.
ARSENAL YAMGEUKIA LOOKMAN
Arsenal wanajipanga kumsajili winga wa Everton Ademola Lookman, kwa mujibu wa The Sun .
Mchezaji huyo wa zamani wa Charlton Athletic amekuwa na wakati mgumu katika Goodison Park licha ya kung'ara kwenye kikosi cha Uingereza U-20 Kombe la Dunia majira ya joto.
UTD KUMRUDIA PERISIC MAJIRA YA JOTO
Man United watarejea majira ya joto msimu ujao na nguvu mpya kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan Ivan Perisic, kwa mujibu wa Gazzetta dello Sport .
MODRIC AVUJISHA SIRI ZA REAL KWA MOURINHO
Luka Modric amekuwa akivujisha taarifa muhimu za Real Madrid kwa bosi wa Manchester United Jose Mourinho, kwa mujibu wa Diario Gol .
Ripoti zinadai kuwa Modric amekuwa akumfahamisha Mourinho kuhusu mambo yanayoendelea kwenye chumba cha kubadilishia nguo Santiago Bernabeu na kuwa Mreno huyo anaweza kutumia taarifa hizo kumnunua Gareth Bale kwa bei pungufu.
NEYMAR AMWINGIZA SANCHEZ KWENYE ORODHA YA PSG
PSG wapo tayari kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, baada ya Neymar kuomba aongezwe kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa kusaijiliwa na klabu hiyo, kwa mujibu waLe Parisien .
SOUTHAMPTON KUMLIPIA £15M WALCOTT
Southampton wapo tayari kutoa paundi milioni 15 kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott Januari, kwa mujibu wa Daily Express .
Walcott pia yumo kwenye rada za Everton, West Ham na Inter, lakini Southampton wanaamini watafanikiwa kumshawishi Muingereza huyo kurejea St Mary's baada ya muongo mmoja tangu ajiunge na Arsenal.
BLIND KUTIMKIA UTURUKI
Fenerbahce inafikiria kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Daley Blind kutoka Manchester United kwa mujibu wa habari kutoka Hurriyet, via Talksport .
Blind anaweza kucheza kama beki wa kati, beki wa kushoto na hata kiungo mkabaji, lakini hana uhakika katika kikso cha Jose Mourinho.
HEYNCKES KURUDI BAYERN
Jupp Heynckes baada ya kustaafu atarejea tena kuinoa Bayern Munich mwisho wa msimu huu kwa mujibu waBild .
Heynckes mwenye umri wa miaka 72 alishinda mataji matatu akiwa na mabingwa hao wa Ujerumani kabla ya kuwasili kwa Pep Guardiola 2013, na atachukua nafasi ya Willy Sagnol anayeiongoza klabu hiyo kwa muda baada ya Ancelotti kutupiwa virago.
Post Comment
No comments