Breaking News

RONALDO ANUKIA MAN UNITED

Cristiano Ronaldo amesema kwamba hataongeza mkataba mpya ndani ya Real Madrid kufuatia kipigo cha goli 3 kwa 0 dhidi ya Tottenham

Spurs wamefanikiwa kufuzu ya 16 bora baada ya ushindi mnono dhidi ya Los Blancos, ambaye pia mambo bado yanamuendea kombo hata kwenye Ligi Kuu ya La liga kufuatiwa kuachwa alama 10 na kinara wa msimamo

Ronaldo bado amebakiza miaka 4 katika mkataba wake anaolipwa paundi 365,000 kwa wiki ambao alisaini mwaka jana, lakini wakati wa mahojiano na beIN Sports baada ya mechi na Spurs Wembley winga huyo amethibitisha kuwa hayuko tayari kumwaga wino ndani ya Madrid kwa mara nyingine

" Siitaji kuongeza. Siitaji kuongeza," alisisitiza. " Nina furaha na mkataba wangu wa sasa niliokuwa nao."

Na alipoulizwa kama ana uhakika", Ronaldo alirudia " Siitaji kuongeza mkataba mpya"

Kumekuwa na taarifa hivi karibuni ziki muhusisha nyota huyo wa Ureno kuwa ana mpango wa kurejea nchini Uingereza kwenye klabu yake ya zamani ya Manchester United

No comments