Breaking News

Mipira ya TFF yaanza kuwaandaa kina Kichuya, Ajib wapya

TFF iligawa mipira katika mikoa mbalimbali ikiwa ni kampeni yake ya kuendeleza na kuibua soka la vijana nchini.

Arusha, Hivi karibuni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liligawa mipira 100 Ukanda wa Kaskazini kupitia kwa mjumbe wao Sarah Chao kwa lengo la kutoa sapoti kwa vituo vya michezo vinavyopatikana Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

Chama cha soka Wilaya ya Arusha Mjini (ADFA) kimefanikiwa kupata mgao wa mipira 15 ambayo imegawanywa katika vituo sita vinavyopatikana wilayani hapa.

Mpira hiyo iwapo itatumika ipasavyo tutarajiwe miaka ijayo kuibuliwa vijana wenye vipaji vipya vya soka watakaoweza kurithi nyayo za kaka zao kama Shiza Kichuya wa Simba na Ibrahim Ajib wa Yanga pamoja na wachezaji wengi wanaotamba katika soka.

Mwenyekiti wa ADFA Omary Walii alisema kuwa kila kituo kimefanikiwa kupewa mipira miwili ambayo ina saizi tofauti, kutokana na umri wa watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo ambavyo vinasai

Vituo vilivyoambulia mipira hiyo ni pamoja na Rollingstone, Future Stars, Tanzanite, Arusha Youth, Nyota Academy, Arusha Soccer, na King Youth Vision Sports Academy huku wakihimizwa kuitumia kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake mkurugezi wa kituo cha Rollingstone Ally Mtumwa alisema kuwa vituo vingi vya michezo havifati misingi mizuri ya kukuza watoto kama kanuni za FIFA na TFF zinavyowahitaji kuzifanya ikiwa pamoja na kuzingatia umri wa watoto.

No comments