Breaking News

#VIDEO- FULL STORY NDOA YA DOGO JANJA NA IRENE UWOYA


Wakati taarifa zikiendelea kusambaa kuhusu Dogo Janja kufunga ndoa na muigizaji Irene Uwoya, msanii huyo ameshindwa kuweka ukweli wa jambo hilo.

Dogo Janja ambaye kwa sasa anafanya vizuri ngoma ‘Ngarenaro’ ameiambia Planet Bongo ya East Africa Radio kwa sasa hayupo Dar es Salaam ila atakaporojea atalizungumzia hilo.
“Nitakuambia tu wala usijali, nikirudi mjini, nipo mitaa ya Bagamoyo, nikitoka naenda Zanzibar, nikitoka nitakupa exclusive” amesema.
Siku ya Jumamosi October 28, 2017 ndipo taarifa zilianza kudai wawili hao kufunga ndoa lakini hakukuwa na ushahidi wowote zaidi ya picha walizoweka katika mtandao wa Instagram ingawa watu karibu na Dogo Janja wamekuwa wakieleza ni kweli.

No comments