Breaking News

UN YATAHADHARISHA KUHUSU HATARI YA KUTOKEA MAUAJI YA KIMBARI

UN yatahadharisha kuhusu hatari ya kutokea mauaji ya kimbari CAR

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusiana na hatari ya kutokea mauaji ya kimbari katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Tahadhari hiyo imetolewa na Adam Ding mshauri maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ofisi ya umoja huo katika kitengo cha "kukabiliana na mauaji ya kimbari" ambaye ametaka kuchukuliwa hatua za kuzuia hilo.

Mshauri huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kitengo cha kukabiliana na mauaji ya kimbari ambaye hivi karibuni alifanya safari katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui ameeleza kuwa, kuna ishara za kutokea mauaji ya kimbari katika nchi hiyo inayokabiliwa na machafuko.

Adam Ding ameongeza kusema kuwa: Baada ya kutembelea nchi hiyo nimeona kuwa, kuna ishara zote za kutokea mauaji ya kimbari katika nchi hiyo ya Kiafrika, kwani kuna vitendo visivyo vya kibinadamu, kumeenea makundi ya wabeba silaha, kuna hatua zinazochukuliwa za kufuta kizazi fulani, serikali ni dhaifu na kunaenezwa ujumbe wa chuki.

Hii si mara ya kwanza kutolewa tahadhari ya hatari ya kutokea mauaji ya kimbari katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Majuma machache yaliyopita pia, Stephen O' Brien Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu alitahadharisha kuhusiana na kuweko ishara za kutokea mauaji ya kimbari katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo inakabiliwa na machafuko.


No comments