Manula amekubali ‘mziki’ wa Nduda
Baada ya Said Mohamed ‘Nduda’ kuonesha kiwango cha juu kwenye mechi ya kutafuta mshindi wa tatu Taifa Stars vs Lesotho, Aishi Manula amemwaga pongezi zake kwa golikipa huyo mzoefu hapa Tanzania.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manula ame-post ujumbe wa kumpongeza Nduda kwa kazi nzuri aliyoifanya na kuisaidia Stars kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya COSAFA 2017.
“Hakika wewe ni bora broo na mara zote umekuwa bora. Kazi uliyoifanya leo ni kubwa mno kwetu watanzania, pia unastahili kupewa pongezi kwa ulichofanya.”
“Kwangu mimi wewe ndio man of the match na ulistahili bro. Keep it up broo @said_nduda”
Dakika ya kwanza tu, Nduda aliokoa mchomo wa Tumelo Khutlang kabla ya kufanya hivyo kwa mshambuliaji huyo dakika ya 10 Stars iliposhambuliwa kwa marabnyingine.
Dakika ya 24 Nduda aliokoa shuti la Jane Thaba-Ntšo wakati Lesotho walipo shambulia goli la Stars wakitafuta bao la kuongoza.
Lesotho waliendelea kuweka presha kwenye lango la Stars na dakika ya 35, Nduda alilazimika kuokoa shambulizi la Thaba-Ntšo kwa mara ya pili.
Kipindi cha kwanza kikamalizika 0-0 lakini Lesotho wakiwa wametawala mchezo kwa kiasi kikubwa.
Lesotho wangepata goli la kuongoza dakika ya 74, lakini Nduda alikua imara kuokoa mpira uliopigwa na Sera Motebang na kuendelea kuiweka Stars salama.
Mechi ikamalizika kwa sare ya bira kufungana na kulazimika kumpata mshindi kwa mikwaju ya penati. Nduda akapangua penati ya Thapelo Mokhehle, kisha Raphael Dauidi akafunga mkwaju wa mwisho na kuipa Stars ushindi wa penati 4-2.
Manula amecheza mechi tano katika mashindano hayo (mechi tatu hatua ya makundi, mechi ya robo fainali na nusu fainali) huku Nduda yeye akicheza mechi ya mshindi wa tatu.
No comments