Manchester City kumuuza Wilfried Bony
London, England. Miamba ya Ligi Kuu England, Manchester City wametangaza dau la mchezaji wake anayetakiwa kuondoka kikosini hapo.
Klabu hiyo imesema mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast, anaweza kusajiliwa kwa dau la Pauni 17.5 milioni.
Kwa maana hiyo, thamani ya mchezaji huyo imeshuka kwa zaidi ya Pauni 10 milioni ndani ya kipindi cha miaka miwili na nusu tangu aliposajiliwa Manchester City akitokea Swansea.
Bony (28) alicheza msimu uliopita kwa mkopo kwenye klabu ya Stoke City, baada ya kutokuwapo kwenye mipango ya kocha Pep Guardiola.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Swansea anatajwa kutimkia Uturuki klabu za Besiktas na Fenerbahce.
No comments