Breaking News

POLISI WAENDELEA KUMHOJI PONDA

Sheikh Ponda Issa Ponda anaendelea 'kusota' rumande katika kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda anaendelea 'kusota' rumande katika kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Ponda alijisalimisha jana Ijumaa kituoni hapo kuitikia wito wa kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa aliyemtaka kuripoti ndani ya saa 72 akimtuhumu kutoa lugha za kichochezi.

Mara baada ya kuripoti jana, alifanyiwa mahojiano yaliyodumu  siku nzima kisha polisi walikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi, Kamanda Mambosasa amesema atalizungumzia suala hilo baadaye baada ya kupata taarifa za suala hilo.

Msemaji wa jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimba ameliambia Mwananchi kuwa ukaguzi ulifanyika jana usiku nyumbani kwa Sheikh Ponda kisha akarejeshwa kituoni.

"Suala la dhamana bado ni gumu, lakini mawakili wetu wanasema wanalifanyia kazi na lolote linaweza kutokea tumwombe tu," amesema Sheikh Katimba

Jana Jumamosi, mmoja wa mawakili wa Ponda, Yahaya Njama amesema mteja wake alihojiwa kwa tuhuma za uchochezi za kuchochea watu waweze kufanya jambo baya.

No comments