Chadema yatangaza wagombea uchaguzi mdogo wa madiwani
Uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 nchini unafanyika Novemba 26,2017.
Arusha. Chadema imepitisha wagombea 16 wa udiwani katika uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyika Novemba 26,2017.
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa amesema wagombea hao wameshapitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Amesema katika Kata ya Murieti iliyopo jimbo la Arusha Mjini aliyepitishwa ni Simon Mollel na Kata ya Moita, jimboni Monduli aliyeteuliwa ni Lobolu Lerango.
Golugwa amesema katika Kata ya Musa iliyopo Halmashauri ya Arusha aliyepitishwa ni Elihud Laizer.
Katika Halmashauri Meru, amesema waliopitishwa na kata zao zikiwa kwenye mabano ni Dominick Mollel (Ambureni), Joyce Ruto (Makiba), Asantaeli Mbise (Maroroni), Daniel Mbise (Leguruki) na Emmanuel Salewa (Ngabobo).
Katika Jimbo la Hai, waliopitishwa ni Elibariki Lema (Machame Magharibi), Moses Kalage (Weruweru), Ezra Ngapi (Mnadani) na Heldak Minde (Bomambuzi).
Amesema mkoani Tanga, aliyepitishwa ni Josiah Shemeta (Lugusa) na Jafari (Ndege Momba).
Kata ya Majengo wilayani Korogwe aliyepitishwa ni Abdallah Maoga na katika
Kata ya Nangwa wilaya Babati aliyepitishwa ni Yohana Dafi.
Akizungumza uchaguzi huo, Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amesema wamejipanga kurejesha kata zote tano katika jimbo lake.
"Tumejipanga kufanya kampeni za kistaarabu na tuna uhakika wa ushindi," amesema.
No comments