Alichokisema Kigwangalla Kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema…>>>”Asante Mungu kwa neema yako. Madaktari bingwa wa Macho kutoka Hospital ya Muhimbili, Hindumandal na Ebrahim Haji. Wameendelea kutimiza ahadi yao kutokana na zoezi letu la upimaji pamoja na matibabu ya Macho.”
“Gharama za upasuaji wa Macho ni kati ya Shillingi 900,000 hadi 1,000,000 pamoja na Miwani hivyo kwa Watu 1,000 ni sawa na Kiasi cha Shilling Billion Moja lakini kupitia wadau Wagonjwa hao watapatiwa matibabu na Miwani Bure ili waone Matunda ya Serikali ya awamu ya Tano kupitia RC Makonda. Mungu wangu atukizwe daima.”
Baada ya ujumbe huo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, ustawi wa jamii, jinsia, wazee na watoto Dr Hamisi Kigwangalla akamuandikia ujumbe uliosomeka…>>>”Mdogo wangu Paul Makonda, hii ni kazi ya utumishi kwa wanadamu hapa duniani leo hesabu imeandikwa kesho akhera! Mungu akubariki kwa kuwezesha kurudisha matumaini kwa wenzetu…Amina!”
No comments