Breaking News

WAZIRI KIGWNGALA AMJIBU KIKWETE

Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Khamis Kigwangalla amefunguka na kudai haoni ajabu yeyote kwa Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kupinga mtazamo wake, wala haimanishi kwamba wanaugomvi.


Hatua hiyo imekuja baada ya Dkt. Kigwangalla kuweka ujumbe katika ukurasa wake wa twitter akitoa maoni yake juu ya usaili wa awamu ya kwanza kwa wanaotafuta ajira katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliyofanyika Agosti 30, 2017 na kupelekea Mbunge Ridhiwani Kikwete naye kutoa maoni yake juu ya hicho jambo ambalo watu wengi walihisi pengine wawili hao wanachukiana kwa namna moja ama nyingine.
Kupitia hayo ndipo Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Khamis Kigwangalla naye alipoweza kujitetea kwa upande wake juu ya tukio zima jinsi lilivyotokea.


"Naona wahunzi wa maneno wanaanza kujenga ukuta kati yangu na Ridhiwani kikwete. Sioni nia mbaya kwenye 'comment' yake na wala sina kinyongo naye!.Siyo ajabu mimi na mtani wangu Ridhiwani ama mwanaccm yeyote yule kuwa na mitazamo tofauti kwenye suala la ajira, hiyo haimaanishi tuna ugomvi", aliandika Dkt. Kigwangalla.
Pamoja na hayo, Dkt. Kigwangalla aliendelea kwa kusema "viongozi wa CCM (wenye dola) ni vizuri tukijadili suala la changamoto ya ajira kwa sababu tuna nafasi ya kushawishi suluhu ndani".
Kwa upande mwingine, Dkt. Kigwangalla amesema katika changamoto kubwa ambazo viongozi wa leo wanakupambana nazo ni pamoja na suala zima la ajira

No comments