BAADA YA KUCHANWA, KANYE AJITOA TIDAL
AMEJIKATAA KIBISHI! Huku zikiwa zimepita siku kadhaa tangu Jay Z alipotoa albamu yake ya4:44 na kumchana mshikaji wake, Kanye West, hatimaye mwanamuziki huyo amejiondoa rasmi katika mtandao wa kuuza ngoma, Tidal ambapo pia Jay Z ana share zake huko.
Za chinichini zinasema kwamba baada ya kutoa albamu yake ya Life Of Pablo, mtandao huo ulipata watu takribani milioni 1.5 lakini cha ajabu hakupewa malipo yaliyotokana na wingi wa watu hao kitu kilichopelekea kuamua kujiondoa tu kwani haoni faida yoyote ile.
Unajua nini? Wakati uamuzi wake ukiwa umewekwa hadharani, maoni ya wadau wengi wamesema kwamba chanzo si hiyo albamu yake ya Life Of Pablo bali ni kuchanwa kwenye ngoma ya Kill Jay Z kwani kama ishu ni malipo, kwa nini hakudai malipo kipindi cha nyuma mpaka albamu ilipotolewa? Mwaka huu tutaona mengi sana.
No comments