Breaking News

WANANCHI WAFURIKA KUPIMA AFYA BURE MNAZI MMOJA-DAR


Wananchi mbalimbali wakazi wa Dar es Salaam wamejitokeza katika zoezi la Upimaji wa Afya Bure kwa muda wa siku tano limeanza leo Septemba 6 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo baadhi ya wananchi wamewahi kwenye viwanja hivyo tokea saa 10 usiku. 

Mwamko huu ni baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutangaza zoezi la upimaji bila Malipo. 

Madaktari bingwa na wauguzi kutoka hospitali za Umma, jeshi na zile za watu binafsi wanaendelea na zoezi la upimaji kwa wananchi. 

Katika upimaji huo mwananchi atakaepimwa na kubainika kuwa na matatizo ya kiafya atapelekwa hospitali na kupatiwa matibabu bure.






No comments