WATEKAJI WA WATOTO ARUSHA WANYONGWE
Mwanasheria wa kujitegemea hapa nchini Alberto Msando, amemtaka Rais Magufuli kusaini hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa wa mauaji ya watoto waliotekwa mkoani Arusha Bw. Samson Peter ili iwe somo kwa wengine.
Kwenye Ukurasa wake wa Instagram Alberto Msando ameandika ujumbe wa kusikitisha kuhusu vifo vya watoto hao waliotekwa na miili yao kukutwa kwenye shimo la choo mkoani Arusha, na kusema kwamba tukio alilolifanya mtuhumiwa huyo ni la ukatili wa hali ya juu, na kwamba kesi yake iendeshwe kwa haraka iwezekanavyo ili ahukumiwe na kumpa adhabu kali ikiwemo kunyongwa hadi kufa.
"Samson Peter Mungu akuadhibu, yaani huyu wala siyo wa kukaa zaidi ya miezi sita na kesi ya utekaji na mauaji!! Hii iishe hata kesho!! Na Rais asaini adhabu ya kunyongwa mpaka afe!! Naomba akihukumiwa tu Mh. Rais atengeneze historia ya kusaini kunyongwa kwake!!!", aliandika Alberto Msando.
Mwanasheria huyo machachari na maarufu Tanzania aliendelea kwa kuwataka wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi katika shughuli ya mazishi ya watoto hao, ili kuwapa faraja wafiwa.
Watoto waliofariki Moureen David na Ikram Salim miili yao iliokotwa jana katika shimo la choo ambako walitelekezwa, baada ya kutekwa na mtu aliyejulikana kwa jina la Samson Peter ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi, kwa tamaa za fedha
No comments