Breaking News

TANZIA : KIPA WA RAYON SPORT AFARIKI DUNIA


KIPA wa kimataifa wa Rwanda na klabu ya Rayon Sports , Mutuyimana Evariste amefariki dunia jana Jumatatu usiku mjini Kigali, Rwanda.
Mutuyimana alifariki nyumbani kwake na baada ya hapo mwili wake ukapelekwa kwenye hospitali ya CHUK  kufanyiwa uchunguzi juu ya kifo hicho.
Kipa huu jana alifanya mazoezi na wenzake siku hiyo na hakuonyesha dalili za tatizo lolote kiafya.
Lakini vyanzo vinasema kipa huyo amekuwa na kawaida kushikwa na magonjwa ya ghafla na iliwahi kumtokea pia akiwa timu hiyo mjini Dar es Salaam mapema mwezi uliopita kwa ajili ya mchezo wa kirafika dhidi ya Simba SC. 

Rais wa timu Rayon Sports, Gacinya Chance Denis ameiambia  kwamba magonjwa hayo humshika usiku.

“Ana kawaida ya kushikwa na magonjwa ya ghafla, yalimshika usiku akiwa mwenyewe nyumbani, tulimpeleka kwenye hospitali, lakini bado kitu kilichosababisha kifo chake hakijajulikana.” Alisema Gacinya alieleza
Mutuyimana Evariste alijiunga na timu ya Rayon Sports mwaka uliopita kutoka nchini Kenya alipokuwa anachezea Sofapaka


No comments