Breaking News

"GOOD NEWS" KUTOKA VISIWANI ZANZIBAR

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud amepiga stop Mpango wa utozwaji Tozo kwa vyombo vya moto viingiavyo katika Mji Mkongwe mpaka pale Serikali itakapotafakari kwa kina na pia kufanya Vikao na wadau wote wa Mji Mkongwe wakiwemo wakazi kuangalia na kushauriana namna bora ya kuendesha zoezi ilo.

Mh. Ayoub ametoa zuio hilo kufatia Malalamiko na tafrani iliyoonyeshwa na wananchi mara tuu baada ya kutolewa tangazo hilo hapo jana.

Akizungumza na wakazi wa Mji Mkongwe ambao  ambao walizuia Msafara wake na kumuomba atoe ufafanuzi kufatia tahaluki  iliyojitokeza tokea ilipotoka taarifa ya Mamlaka ya Mji Mkongwe,Mkuu wa Mkoa amesema Serikali ya Mapinduzi kupitia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ally Mohamed Shein siku zote inajali na kushughulikia matatizo ya wananchi wake na pia kutafuta namna bora ya kuwapunguzia wananchi ugumu wa maisha na sio kuwaongezea,Amesema Serikali italiangalia suala hili kwa kina kabla ya kufikia Maamuzi.

Taarifa hiyo iliyotolewa hivi karibuni na inayosambaa kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii ilidai kuwa Kutokana na agizo la Serikali la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka ya Mji Mkongwe: Kuanzia tarehe 06/09/2017 kutakuwa na mabadiliko ya Uingiaji na Utokaji wa Mji Mkongwe kama ifuatavyo:-

1:Kuingilia itakuwa ni njia ya Malindi badala ya njia ya Haele Salase/Vuga.

2: Gari za kawaida zitalipa Sh.3000 za kuingilia (intrence fees).

3: Gari za Tax na Private Hire zitalipa Sh.5000.

4:Gari zote za Mabasi ya kuchukulia Wageni pamoja na Gari za Mizigo ni Sh.10,000.

Hivyo Mh. Ayoub Amesitisha Mara moja tozo hizo na kuzitaka mamlaka husika kushirikina na wadau na wananchi.

Hata hivyo kupitia mitandao yake rasmin ya kijamii Mh. Ayoub Mahmoud alionekana kuweka wazi taarifa yake kwa kuandika kwenye kurasa zake za instagram na Facebook maandishi yenye maneno ya kuwataka wananchi watulie hadi pale serekali itakapo toa ufafanuzi.

No comments