Breaking News

Julio: ‘Nipeni mechi 3, Dodoma FC itacheze Ligi Kuu’

Kocha Dodoma FC, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ amesema anataka mechi tatu (3) za kirafiki kabla ya kuanza kwa Ligi Daraja la Kwanza Septemba 16, itakuwa tiketi ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao. 

Julio alisema timu hiyo ipo tayari kwa ligi baada ya kujifua kwa muda mrefu ikiwa kambini Chuo kikuu Dodoma {Udom}, lakini kilichobaki ni kucheza mechi 3 tu za kirafiki kujiweka sawa kabla ya ligi kuanza. 

 “Baada ya kucheza na Singida United,bado ninahitaji zaidi ya mechi hizo zitanipata muunganiko ninaoutaka kwani tumejifua vya kutosha sana kilichobaki ni mechi hizo tu baada ya hapo lengo la timu litatimia.” 

Katika hatua nyingine Julio alibainisha kuwa faida za kucheza mechi hizo ni kutambua mapungufu ya timu ndio maana baada ya mchezo dhidi ya Singida United waliofungwa mabao 3-0 aligundua safu yake ya ulinzi inahitaji marekebisho zaidi kutokana na makosa waliyoyafanya na tayari ameshafanyia kazi na atathibitisha kupitia mechi za kirafiki. 

 Katibu wa Dodoma FC, Fottunatus John alisema kesho Alhamisi wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Area C inayoshiriki ligi daraja la pili katika uwanja wa Jamhuri mjini hapa kabla ya kucheza mechi nyingine 2 wiki ijayo.

No comments