Breaking News

WYNE ROONEY AKAMATWA

Mshambuliaji wa Everton amekamatwa kwa kushukiwa kuendesha gari akiwa “amelewa”, kwa mujibu wa wa mtandao wa BBC. Rooney alisimamishwa na polisi karibu na nyumbani kwake eneo la Cheshire siku ya Alhamisi usiku.

Mshambuliaji huyo, 31, alitangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa wiki iliyopita, baada ya kuichezea timu ya taifa mara 119 na kupachika mabao 53.

Alijiunga tena na Everton msimu huu akitokea Manchester United, na kufunga katika mechi zake mbili za Ligi Kuu ya England. Alifunga pia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia nchini Tanzania.

No comments