Breaking News

MBOWE:HAKUNA UTARATIBU WA KUMSAFIRISHA LISSU

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu

Akizungumza leo Ijumaa jijini hapa, Mbowe amesema madaktari wamesema hawezi kwenda popote kutokana na hali yake.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kwa sasahakuna utaratibu wa kumsafirishaMbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwenda Marekani au Ujerumani kutokana na ushauri wa madaktari wanaomtibu.

Akizungumza leo Ijumaa jijini hapa, Mbowe amesema madaktari wamesema hawezi kwenda popote kutokana na hali yake.

Amesema baada ya awamu ya kwanza ya matibabu aliyoyapata katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7, ya pili inafanyika Nairobi, Kenya alipo sasa.

"Awamu ya tatu itaamua aende wapi ambayo itahusu mazoezi," amesema Mbowe.

No comments