Breaking News

NG'OMBE ASABABISHA AJARI NA KUUA MTU MMOJA

 Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine sita wamejeruhiwa huku watu zaidi ya 50 wakinusurika kifo baada ya ajali iliyosababishwa na ng'ombe aliyekuwa akivuka barabara ghafla bila kuonekana na dereva wa basi la kampuni ya Kidia One.

lililokuwa linatokea Dar kwenda Mwanza.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi SSP Elias Mwita Mkoa wa Shinyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambaopo amesema ajali hiyo imetokea eneo la tinde nyuma kidogo kabla ya kufika Mkoa wa Shinyanga.

Akielezea mazingira ya ajali hiyo Kaimu Kamanda Mwita amesema ng'ombe alitokeza na kuvuka barabara ghafla huku ikidaiwa kuwa dereve alikuwa hajamuona na alipomuona alikuwa akijitahidi kumkwepa hali iliyosababisha apoteze uelekeo na kupelekea gari kupinduka na kusababisha kifo pamoja na majeruhi.

Hata hivyo Kamanda Mwita amesema majeruhi sita wapo hospitali wakipatiwa matibabu lakini dereva ametorokea kusikojulikana ingawa wanaimani kama Jeshi la polisi hadi kufikia leo mchana watakuwa wameshamkamata.

No comments