Breaking News

ESTER BULAYA AFUNGUKA YA MOYONI


Mbunge wa Bunda Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Ester Amos Bulaya.

Mbunge wa Bunda Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Ester Amos Bulaya amefunguka kwa kuwashukuru wananchi wa Bunda, Mara na Watanzania kiujumla kwa kuacha kufanya mambo yao na kumuombe yeye kipindi alipokuwa anaumwa.

Bulaya ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa twitter ikiwa zimepita wiki mbili tokea Mbunge huyo kuzidiwa na kupelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi baada ya kupewa rufaa katika hospitali aliyokuwa amelazwa awali ya Mkoa wa Mara.

"Namshukuru Mungu naendelea vyema, asanteni wanabunda, Mara na Watazania wote kwa maombi yenu, afya yangu inazidi kuimarika. 'God is good", aliandika Bulaya.


No comments