Breaking News

DAKTARI AELEZA NAMNA MANJI ALIVYO ZIMIA MAHABUSU.

Daktari Mfawidhi wa Gereza la Keko, Inspekta Eliud Mwakawanga leo September 26, 2017 ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi maisha ya mfanyabiashara Yusuf Manji yalivyokuwa gerezani, akisema alikuwa anatumia vidonge kati ya 25 mpaka 30 kwa siku.

Inspekta Mwakawanga amedai walikuwa wakimpatia dawa hizo iwapo akisikia maumivu hasa ya mgongo na kuna kipindi anachoamka anakuwa katika hali ya kutetemeka au kuchanganyikiwa.

Aidha, alidai kuna wakati alikuwa anaamka anashindwa hata kutembea na wakati mwingine alikuwa akitumia mkanda wa kufunga mgongo.

Shahidi huyo wa sita wa upande wa utetezi alidai July 6, 2017 walimpokea Manji akitokea Hospitali ya Muhimbili Kitengo cha moyo cha JKCI ambapo waliambiwa ni mshtakiwa lakini ni mgonjwa na alienda kumuona na walikaa naYe gerezani hadi alipokuja kuachiwa.

”Tangu nimempokea hali yake kiafya haikuwa nzuri na alikuwa mtu anayetumia dawa wakati wote na alikuja na dawa zake za aina sita kutoka Muhimbili ambazo alikuwa akizitumia. Pia kulingana na hali yake na mazingira anayokuwa anajisikia, tulikuwa tukimpatia dawa gerezani mbali na hizo.”

Alidai utaratibu wa kuwapatia dawa mahabusu na wafungwa, dawa wanakaa nazo wao wataalam na wanawapa kutokana na maelezo ya daktari yaliyopo kwenye cheti ambapo Manji kuna dawa alikuwa anakunywa asubuhi na jioni na nyingine kulingana na hali yake ya siku hiyo.

Shahidi huyo alidai kuwa wao hawatoi dawa za kulevya kwa mgonjwa ila wanatoa dawa ambapo baada ya kuulizwa na Wakili Hajra Mungula kuwa dawa walizompatia Manji zinahusiana vipi na dawa za kulevya.

”Sijachunguza sana kuona zina uhusiano gani na dawa za kulevya na kusisitiza wao hawatoi dawa za kulevya kwa mgonjwa wanatoa dawa.”

No comments