Breaking News

Maalim Seif alimaliza mgogoro wa madiwani Tanga kimyakimya

Mbarouk alisema Maalim Seif alikaa na madiwani hao jijini Dar es Salaam na kuwaamuru waingie kwenye vikao vya Halmashauri ya Jiji la Tanga ili kuwaletea maendeleo wananchi.
 Mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbarouk amesema mgogoro wa madiwani wa CUF umemalizwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.
Mbarouk alisema Maalim Seif alikaa na madiwani hao jijini Dar es Salaam na kuwaamuru waingie
kwenye vikao vya Halmashauri ya Jiji la Tanga ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Mbunge huyo ambaye wiki iliyopita alituhumiwa na baadhi ya madiwani waliosimamishwa kuhusika kumchochea Meya wa Jiji la Tanga, Mhina Mustafa (Selebosi) kuwapa adhabu hiyo, alikanusha tuhuma hizo.
CUF ina madiwani 20 ambao kati yao, 12 waliamua kuingia kwenye vikao vya Baraza la madiwani mwaka jana na kutuhumiwa kukisaliti chama, lakini baadaye wenzao wanane nao waliingia huku wakilalamika kutengwa na kunyimwa stahiki zao.
Naye Naibu Meya wa Jiji la Tanga, Mohamed Haniu (CUF) alisema kitendo cha madiwani 20 wa CUF kuingia kwenye vikao kimesababisha wenzao na wale CCM kuelekeza nguvu zaidi kwenye maendeleo.

No comments