Breaking News

Wananchi waliojichukulia sheria mkononi jana  wamewaua kwa kuwachoma moto watatu

Wananchi waliojichukulia sheria mkononi jana  wamewaua kwa kuwachoma moto watu watatu ambao majina yao bado hayajafahamika katika kijiji cha Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama,mkoani Shinyanga kwa tuhuma za wizi wa pikipiki. 

Kwa mujibu wa mashuhuda, mauaji ya mtu wa kwanza yalifanywa majira ya saa nane usiku wa kuamkia jana baada ya kutokea wizi wa pikipiki, huku watu wengine wawili wakiuawa jana  majira ya saa nne asubuhi. 

Inaelezwa kuwa mtuhumiwa wa kwanza alipokamatwa aliwataja wenzake wawili waliouawa jana baada ya kuvunja nyumba ya mmoja wao na kukuta pikipiki tatu zimehifadhiwa kwenye shimo. 

Afisa mtendaji wa mtaa wa Kitwana, Peter Joseph amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akilaani vikali kitendo cha wananchi kujichulia sheria mkononi, na kuwataka kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha sheria. 

Miili ya marehemu hao ilichukuliwa na Jeshi la polisi wilaya ya Kahama, na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama 


No comments