JINSI YA KUNG`ARISHA MENO YAKO
Hakuna mtu anapenda kuwa na meno ya njano, japokuwa wengine ni Matatizo ya kimazingira kama watu wa Kaskazini mwa Tanzania, kule Arusha, Kabla sijasema nini cha kufanya meno yako yabadilike na kuwa na rangi nyeupe, kwanza tuongelee vitu vinavyo sababisha meno kubadilika rangi,
Matumizi ya tumbaku au kuvuta sigaraAina ya vyakula na vinywaji vya rangi, kama soda,Kahawa chai ya rangiBaadhi ya magonjwa na dawa kama (Antibaotics)Vina saba, baadhi ya watu meno yao kiasili sio meupe kama wengineMaradhi ya kinywaMazingira
Sasa nini cha kufanya kun’garisha meno yako ukiwa nyumbani, kuna vitu kadhaa unaweza kutumia ambavyo ni,
Baking Soda/Bicarbonate of Soda wengi tunaijua inatumika kwenye kupikia vitu vya ngano ngano, kama keki, au maandazi chukua baking soda yako kijiko kimoja changanya na maji ya limao/ndimu kupata mchanganyiko wenye kuweza kupaka kwenye meno kisha pakaa kwenye meno yako huku ukisugua meno yako, unaweza kupaka na kitambaa au ukatumia mswaki au kidole kisafi . Acha ikae dakika 2 tu kisha sukutua na maji safi kisha piga mshwaki kawaida. Unaweza kutumia mara 4 kwa wiki kwa kuruka siku 1 baada ya siku uliyoanza kutumia, mpaka utakapo pata matokeo unayoyataka, NB: Kumbuka ni Baking Soda/Bicarbonate of Soda na sio Baking Powder hii haifai na inaweza kuharibu fizi na kinywa chako.
Mafuta Ya Nazi/ Mafuta ya Mzaituni (Olive oil) sasa usije ukapaka yale ya Nywele, kama unao uwezo wa kutengeneza mafuta yako ya nazi basi itakuwa raisi, unaweza tumia hayo ya kiasili kuliko ya viwandani. Utaweka mafuta yako kwenye kitambaa na utasugua meno yako fanya mara kwa mara mpaka upate Utafanya hivyo kwa mafuta ya mzaituni pia.
Maganda ya chungwa au Ndizi. Sugua meno yako na sehemu ya ndani ya maganda ya chungwa au Ndizi madini yanayopatikana katika maganda haya kusaidia meno yako kuwa meupe.
Kula Matunda, kama strawberries, Apple, karoti ni aina ya matunda ambayo husaidia kuboresha meno yako,na vitamin c iliyopo kwenye matunda haya itasaidia kutoa harufu mbaya mdomoni.
Tumia mrija, kama unakunywa vinywaji kama soda, hii itasaidia kupunguza uwezekano wa kubadilika kwa rangi ya meno yako, ikiwezekana punguza kabisa unywaji wa soda nyeusi na vinywaji kama kahawa na chai ya rangi.
Zipo njia za kitaalamu za kun’garisha meno ambazo zinafanyika katika hospitali mbalimbali, kama utaona kuna ulazima nenda kamuone daktari, zingatia kumuona Daktari wa Meno mara kwa mara, kwa ushauri juu ya magonjwa ya kinywa na jinsi ya kujikinga na maradhi na kutunza meno yako.
No comments