Vituo vya mafuta kuendelea kufungwa
Kwa mujibu wa TRA zoezi hilo litakuwa ni endelevu na la nchi nzima ili kuhakikisha sheria inafuatwa.
Dar es Salaam. Vituo kadhaa vya kuuza dizeli, petroli na mafuta ya taa vimefungwa jijini hapa kutokana na kutokuwa na mashine za kielektroniki za kutoa risiti (EFDs).
Hatua hiyo inayotekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeelezwa kuwaathiri si tu wenye vituo bali hata watumiaji.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amesema leo Julai 14 na kuongeza kwamba wanaendelea na kazi hiyo nchi nzima ili kuhakikisha sheria inatekelezwa.
No comments