UJIO WA BARCELONA ENGLAND WAMTISHA WENGER
Baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Brighton and Hove Albion, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ujio wa Barcelona katika Ligi Kuu England itaongeza ugumu kwa kila timu.
Akizungumzia hilo kutokana na hali ya kisiasa ilivyokuwa kwa sasa Catalonia, na kumekuwa na tetesi kuwa ni wapi Barcelona itacheza kama wakiondolewa kushiriki LaLiga.
Wenger aliuliza kuhusu mtazamo wake iwapo timu hiyo itapendelea kucheza katika Ligi Kuu England.
London, England.Baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Brighton and Hove Albion, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ujio wa Barcelona katika Ligi Kuu England itaongeza ugumu kwa kila timu.
Akizungumzia hilo kutokana na hali ya kisiasa ilivyokuwa kwa sasa Catalonia, na kumekuwa na tetesi kuwa ni wapi Barcelona itacheza kama wakiondolewa kushiriki LaLiga.
Wenger aliuliza kuhusu mtazamo wake iwapo timu hiyo itapendelea kucheza katika Ligi Kuu England.
ADVERTISEMENT
"Najaribu kujifunza kwa kinachotokea Catalan," alisema Wenger.
"Kama Barcelona wanataka kujiunga na Ligi Kuu England, itafanya mambo kuwa magumu kwa kila mmoja wetu.
"Lakini sihamini kama watafikia hatua hiyo.
"Ni jambo linalovutoa na linatokea katika michezo hasa Barcelona ambayo imekuwa ni timu ya kisiasa zaidi."
Wakati alipoulizwa tena kama yuko tayari kuwakaribisha Barcelona katika Ligi Kuu England, Mfaransa huyo alidai kuwa wanatakiwa kuangalia timu zilizokuwa karibu na nyumbani kwao kwanza kama wanampango huo.
"Nafikiri itakuwa vizuri kuwaona jinsi watakavyopambamba katika Ligi Daraja la kwanza," aliongeza.
"Hapa tuna idadi ya timu za kutosha 20, lakini kama wanataka kuongeza kufikia 24, tulitakiwa kwanza tukaribishe klabu kutoka Scotland kabla ya kwenda Hispania."
No comments