Breaking News

Tanzania yapaa FIFA

Timu ya Tanzania, Taifa Stars.

Tanzania imepaa kwa nafasi 25 hadi nafasi ya 114 kutoka nafasi ya 139 kati ya mataifa 211 katika viwango vya ubora wa soka duniani vilivyotolewa na FIFA leo Julai 6, 2017. 

Hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikicheza katika kiwango kizuri ambapo iliwashinda Botswana na Burundi katika mchezo wa kirafiki,  Malawi pamoja na Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana katika michezo ya COSAFA inayoendelea. 

Katika viwango hivyo vipya vya mwezi Julai, Germany imeishusha Brazil kileleni na kukamata usukani rasmi wa dunia, huku Brazil ikishuka hadi nafasi ya pili na Argentina imeporomoka na kufikia nafasi ya tatu. 

Katika 'top ten' mataifa yanayofuata ni Ureno, Uswisi,Poland, Chile, Colombia, Ufaransa na Ubelgiji inakamata nafasi ya 10. 

Barani Afrika Misri inaongoza ikiwa nafasi ya 24 ikifuatiwa na Senegal katika nafasi ya 27, Congo DR nafasi ya 28, Tunisia nafasi ya 34, Cameroon nafasi ya 36, Nigeria nafasi ya 39 huku Burkina Faso akiangukia nafasi ya 44. 

Kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda imeporomoka nafasi tatu mpaka kufikia 74, ikifuatiwa na Kenya kuanguka nafasi 10 mpaka 84, Tanzania imepanda nafasi kwa nafasi 25 juu mpaka kufikia 114, Burundi ikipanda nafasi 27 juu na kufikia 121, Rwanda imepanda nafasi moja na kufikia 127, Ethiopia ikidondoka kwa nafasi 11 na kufikia 136. 

Wengine ni Djibouti ambayo iko nafasi ya 185 huku Eritrea na Somalia zikiwa mkiani kabisa katika nafasi ya 206

No comments