Baada ya ishu ya Yanga kubuma, Ngassa aamua kujifua Mwanza
Baada ya mipango ya kurejea "kubuma", Mrisho Ngassa ameamua kujifua vilivyo kwao jijini Mwanza.
Ngassa alitaka kurejea Yanga lakini ilionekana hakuwa amefuata utaratibu sahihi na uongozi wa juu ukamzuia.
Naye ameamua kujifua vilivyo Mwanza ambako amekuwa akifanya mazoezi makali mchangani na wakati mwingine milimani.
Ngassa ambaye alijiunga na Mbeya City kwenye dirisha dogo la msimu uliopita akitokea Fanja ya Oman, alikuwa na wakati mgumu kwenye kikosi hicho, ambapo tangu alipojiunga nacho, hakuwa na mwendelezo wa kupachika mabao kama ilivyokuwa zamani alipozitumikia Simba, Yanga na Azam FC.
No comments