SETHI AUGUA, KESI YAKE NA RUGEMALIRA YAAHIRISHWA
James Rugemalira(mwenye mvi) na mwenzake Harbinder Singh Sethi wakifikishwa mahakani leo.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kesi inayowakabili mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemalira wanaokabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara.
Rugemalira na Harbinder Singh Sethi baada ya kutoka kortini.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 22, mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa serikali, Leornad Swai, kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Mawakili wanaomtetea mfanyabiasharaHarbinder Singh Sethi wameiomba Mahakamaimruhusu mteja wao akatibiwe nje ya nchi, kutokana na kuwa na uvimbe na Baloon tumboni hali inayomsababishia maumivu makali na kumnyima usingizi kwa wiki ya nne sasa, ombi ambalo limekataliwa na Mahakama na kuagiza atibiwe Muhimbili.
No comments