Serikali kuwaondoa wabadhirifu vyama vya ushilika
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Rais John Magufuli haitamuonea haya mbadhirifu yeyote wa mali na fedha za vyama vya ushirika nchini.
Aliyasema hayo jana (Jumamosi) katika maadhimisho ya Siku ya Ushirika Dunia, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Dodoma.
Alisema changamoto nyingine zinazo vikumba vyama hivyo zinachangiwa na baadhi ya viongozi wake kutoheshimu miongozo ya vyama vyao na kujifanyia mambo kwa maslahi binafsi.
Majaliwa alisema katika kukabiliana na changamoto hizo, Serikali itaendelea kutimiza wajibu wake na kuweka mazingira rafiki ya kustawisha Ushirika nchini ili kutoa fursa ya kushamiri na kuwawezesha Watanzania kumiliki uchumi wa nchi yao.
Pia, alizielekeza Kamati za Ushauri za mikoa na wilaya nchini, zihakikishe sekta ya Maendeleo ya Ushirika inafanywa ajenda muhimu inayopaswa kujadiliwa na kuwekewa maazimio ya utekelezaji. Hata hivyo, Waziri Mkuu alizielekeza mamlaka zote zinazohusika na Ushirika nchini, zijiwekee malengo yanayopimika ya namna ya kuboresha sekta hiyo.
No comments