Breaking News

Polisi wamkamata Halima Mdee nyumbani kwake

Kwa ufupi

Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) amekamatwa kwa maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi akidaiwa kumkashifu Rais.

By Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz

 Mbunge wa Kawe, Halima Mdee amekamatwa na polisi wanne na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay saa  moja iliyopita.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo, amezungumza na Mwananchi  saa 12 jioni na kueleza kuwa Mdee amekamatwa akiwa nyumbani kwake Makongo Juu.

 Awali akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi,  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi aliagiza Jeshi la Polisi kumkamata mbunge huyo  kwa madai kuwa amemkashifu Rais John Magufuli.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya  hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.

“Wapi kakamatwa? Sisi tunachojua ni kuwa tunatekeleza agizo la DC (mkuu wa wilaya) mengine muulize kamishna wa kanda maalum, nimetimiza,” amesema.

No comments