Malinzi na wenzake kusota lumande hadi Julai 17
Rais wa TFF, Jamali Malinzi na wenzake wataendelea kusota Lumande hadi Julai 17, 2017 bila kesi yao kutajwa, kufuatia upande wa Jamhuri kushindwa kukamilisha upelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.
Wakili wa Serikali Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri, leo Julai 3,2017 mahakamani hapo, alida kuwa Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuiomba Mahakama kupanga tarehe ya kutajwa kesi hiyo.
Ndipo Hakimu Mashauri aliipanga Tarehe 17 Julai mwaka huu, kuwa siku ya kutajwa kesi hiyo.
Jamali na Wenzake akiwemo Katibu Mkuu wa TFF, Selestin Mwesigwa walitiwa mbaroni na Takukuru kwa tuhuma za Uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi, na kufikishwa kizimbani leo Julai 3, 2017.
No comments