MAGUFULI AZINDUA BARABARA YA KAGOMA-BIHARAMULO-LUSAHUNGA
Rais Dkt. John Magufuli akipeana mkono na Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa baada ya kuzindua barabara hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Barabaraya Kagoma-Biharamulo-Lusahungaimegharimu Sh 190 bilioni.
Rais John Magufuli akisalimiana na wananchi wa Biharamulo.
Mbarawa ametoa tamko hilo leo wakati akiizindua mbele ya umati mkubwa wa watu ambao walihudhuria uzinduzi wa barabara hiyo ya kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 154.
Rais akiwapungia mkono wananchi wa Biharamulo.
Akizindua ujenzi wa barabara hiyo, Rais John Magufuli amesema kwamba Biharamulo imeshika nafasi ya pili kwa umaskini na wananchi wanafanya ulinganisho na hali ilivyo tofauti katika wilaya jirani ya Chato.
Rais akisalimiana na wazee wa Biharamulo.
Kwa upande wake Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa amesema wanaunga mkono msimamo wa Rais kupiga marufuku wanafunzi wanaobeba mimba kuendelea na masomo na wameanzisha shule ya wasichana ya bweni kuunga mkono kauli yake.
No comments