Breaking News

Kesi ya Manji ya dawa za kulevya yasogezwa Agosti 10

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph  Manji 

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkeha ameiahirisha kesi hiyo leo (Alhamisi, Julai 6) mara baada ya Wakili wa Serikali, Timon Vitalis kudai upelelezi bado haujakamilika. Manji hakuwepo mahakamani.
Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 akidaiwa kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Dar es Salaam. Kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph  Manji imeahirishwa hadi Agosti 10.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkeha ameiahirisha kesi hiyo leo (Alhamisi, Julai 6) mara baada ya Wakili wa Serikali, Timon Vitalis kudai upelelezi bado haujakamilika. Manji hakuwepo mahakamani.

Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 akidaiwa kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, Manji alikana na katika kesi hiyo anawakilishwa na mawakili Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na  Jeremiah Mtobesya.

Manji aliachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye alisaini bondi ya Sh10 milioni.

No comments