Breaking News

Hongera Diamond Platnumz...Ebu Sikia Hawa Wasomi Baada ya Kusikia Diamond Anauza Karanga


Niliwahi kuandika wakati fulani (2015) kuwa ukimwendea Bakhressa ukamwambia kuwa #mihogo ni biashara nzuri atakuita board room muongee vizuri apate kujua vizuri lakini ukimfata msomi mwenye labda masters ya biashara ukamwambia kitu kile kile anaweza kukuona huna idea kichwani. 

Nilipoona video ya #DiamondPlutnumz akizindua biashara yake mpya ya #DiamondKaranga nikawaza tena. Nikamforwadia mdogo wangu mmoja anasoma "ELIMU YA JUU" kwa sasa. Alipoiangalia nikamuuliza maswali machache:

1. Hiyo ni video ya Diamond na karanga? 

Akajibu #NDIYO BRO

2. Nikamuuliza: Diamond amechuja kimuziki ndo maana kakimbilia karanga? 

Akajibu #HAPANA

3. Nikamuuliza: Diamond alisomea biashara Chuo? 

Akajibu #HAPANA

4. Nikamuuliza: Ana akili ya kibiashara? 

Akajibu #NDIYO

5. Nikamuuliza: Ana hela nzuri nzuri benki? 

Akajibu #NDIYO

6. Nikamuuliza: Sasa haoni aibu kuuza karanga? 

Akajibu #HAPANA

7. Nikamuuliza: Kwa nini haoni aibu? Akajibu nadhani sababu ya pale juu NAMBA 4

Nikajisemea: Good.

8. Nikamuuliza: Wewe umesoma kuliko Diamond? 

Akajibu: #NDIYO KAKA.

9. Nikamuuliza: Unaweza kuuza karanga?

......... (KIMYA).......

10. Nikataka kuuliza tena

..nikaona "Typing......" 

Jibu likaja: INATEGEMEA 

Anyway mpaka hapo nikawa nimeelewa jibu sahihi ni lipi. Kwamba nikimpa huyu msomi option mbili baada ya masomo yake. Moja apate AJIRA pale Azikiwe CRDB, mshahara labda laki 9 kwa mwezi na mkopo nafuu wa kununua IST... halafu option nyingine iwe idea ya kuuza karanga kuanzia zero ipi atachagua? 

Nadhani jibu wote tunalo. 

Kuna binti mwingine wa "Elimu ya Juu" alikuja kwangu akiomba msaada wa kutafutiwa mahali pa kufanya kazi kwa muda wakati wa likizo. Pamoja na hilo nilianza kumuuliza kama ana KIPAWA chochote ambacho anaweza kukitumia taratibu akijenge kije kumsaidia baadaye hata ajira zikija kugoma. Pamoja na binti huyo kukiri kuwa anacho kipawa (alinitajia) lakini hakuwa tayari kukifanyia kazi in any way hata kwa muda wa ziada. Anataka tu ajira.

Hili ni #JANGA.

Tuna wasomi wetu wengi ambao wanachotaka ni AJIRA TU. Serikali nayo inadhani itaweza kutatua tatizo la ajira kwa a one-sided view. Kwamba mtu asiye na ajira dawa yake kumpa ajira. Si kweli kwamba hiyo ndo dawa pekee. In fact tuendako hiyo ni wrong solution. Mfano mdogo ajira za madereva kwa dunia ya leo zinaondoka moja moja.

Fikiria: Siku jiji hili la Dar es Salaam kwa mfano hili likiwa na Mwendokasi kila Kona ya jiji na huko mbali na city centre kote kuanzia Bunju (au Bagamoyo) hadi Mbagala na hadi huko Chalinze. 

Halafu treni za umeme ziko 

Halafu self driving cars 

Halafu drones za kudeliver mizigo kwa wateja (yani uko zako nyumbani labda Bunju unaagiza chakula KFC Posta unalipia kwa M-PESA kinaletwa na drone ndani ya robo saa tu hadi mlangoni kwako)

Hapo mtu aliyesomea udereva ataendesha nini? 

Licha ya hayo mambo kukawia yatafika. Lakini hata kabla hayajafika ajira ngapi zipo na nani atapata nani akose.

Wasomi wetu ni lazima waanze kuwaza tofauti na wasomi wa mwaka 1970. Lazima kuwaza option ya kusurvive nje ya mfumo wa ajira. 

Tatizo wengi wanachotaka ni MSHAHARA tu. Ndo maana wakikutana na wewe utasikia: "BRO NIUNGANISHE BASI HATA KWA RAFIKI ZAKO NIPATE KAZI". Ndo lugha yao. NIUNGANISHE. Yaani utadhani wewe umekuwa fundi welding...

Ukimpa idea nyingine HATAKI.

Ndo maana watu wasio na shule ndeefu ndo wanakuwa matajiri. Si bure. Katika matajiri wote 2000+ kwenye Forbes wenye MBA unaweza kuta hata 10 hawafiki. Na hao wenye hiyo MBA siyo kuwa ndo imewafanya wa excel in bness.

Lazima kuwaza kwa mapana. Wasomi hawataki kuumiza kichwa wanataka ready made things. Hii si njema kwa afya ya uchumi wa taifa letu.

Ukitazama #DiamondPlutnumz na karanga unashangaa kwa nini msomi akikuona unaanzisha biashara yako anataka umpe tu AJIRA hataki umfundishe afanye. Makanisani nako wasomi wanaombewa tu wapate AJIRA. Basi. Kweli? Ina maana hakuna MAONO mengine kwa wasomi wetu isipokuwa ajira? 

Elimu ya juu kwa vijana wengi imepeleka creativity yao na uthubutu wao CHINI!

So sad!

Sikiliza kijana msomi: 

Ni muhimu kuyatazama maisha yako kwa mapana na kwa upya kabisa pasipo kuyahusisha na elimu yako ya darasani kabisa. 

Mungu awabariki sana.

Hongera tena #DiamondKaranga


No comments