Breaking News

Kutoka Sengerema: Mwanamke Aangua Kilio Mbele ya JPM

SENGEREMA: Rais John Magufuliamemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela kuyafanyia kazi malalamiko ya mwanamke mmoja mkazi wa Sengeremaaliyedai kunyanyaswa na kuvunjiwa nyumba yake.

Rais ametoa agizo hilo leo(Jumanne Julai 4) wakati akizindua mradi wa maji, wilayani Sengerema na kumtaka Mongela kuchukua namba ya simu ya mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Rosemary Simon, ili atatuliwe tatizo lake.

Kabla ya Rais Magufuli kuchukua hatua hiyo, mwanamke huyo alikwenda mbele ya jukwaa alimoketi Rais, huku akilia kuwa ananyanyaswa na viongozi waChadema na kuwa wanataka kumbomolea nyumba yake, bila kufafanua ni kwa vipi.

“Mpe simu yako Mkuu wa Mkoa, halafu atakutafuta na wala usijali, nitamtuma Mkuu wa Mkoa  na haki yako itatendeka, nitalifanyia kazi suala lako,” amesema Rais.

No comments